Waagizwa kusimamia uuzaji wa mbolea
Mbeya, 6:12:2020 VIONGOZI wa vijiji,mitaa na vitongoji wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameagizwa kusimamia uuzaji mbolea wenye kuzingatia bei elekezi iliyowekwa na Serikali ili kuepusha wakulima kuibiwa na wauzaji wasio waaminifu. Agizo hilo lilitolewa na Kaimu katibu Tawala wa wilaya ya Mbarali,Oliva Sule alipomwakilisha mkuu wa wilaya hiyo Reuben Mfune kutoa salamu za Serikali kwenye Kikao cha kawaida cha Baraza…







