Improving the livelihood of small-scale farmers
Taking a New Look at Africa's Agriculture; Develoepmental Communication

SERIKALI YA TANZANIA YAINGIA MAKUBALIANO NA WAFANYABIASHARA KUPIGA JEKI KILIMO CHA NGANO

DODOMA: 23.01.2021 Serikali imeingia makubaliano na wafanyabiashara ya zao la ngano kuwa wale wote waliokuwa wakiagiza ngano nje ya nchi sasa watanunua asilimia 60 ya ngano hiyo hapa nchini ili kukuza soko la wakulima na kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa bidhaa hiyo. Makubaliano hayo yameingiwa leo Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda na Wafanyabiashara wakubwa wa…

Read More

Homa ya nguruwe yapiga Kanda ya Ziwa

DODOMA: 23.91.2021 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Serikali imeweka mikakati  ya kuhakikisha ugonjwa wa homa ya nguruwe ulioikumba mikoa ya Kanda ya Ziwa hivi karibuni unadhibitiwa. Aidha alisema tangu ugonjwa huo uanze mpaka sasa umeshasababisha vifo vya nguruwe 1,500 wenye thamani ya shilingi milioni 375. Ndaki aliyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa…

Read More

Serikali ya tanzania yaahidi nguvu zaidi uzalishaji alizeti

DODOMA: 22.1.2021 SERIKALI imesema ina mpango wa kuongeza nguvu uzalishaji wa zao la alizeti kwa lengo la kuhakikisha kuna mafuta ya kutosha ya kula yanayozalishwa nchini na hivyo kupunguza utegemezi wa mafuta hayo kutoka nje. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo sasa uzalishaji wa ndani  unakidhi asilimia 43. Aidha nchi inazalisha tani  270,000 za mafuta ya kula kila mwaka  na…

Read More

Wasindika mchele na soko la Afrika mashariki

KAHAMA: 21.1.2021  WASINDIKAJI wa mchele  wameitaka serikali kufungua soko la EAC na SADC  ili waweze kuwa na bei yenye ushindani. Imeelezwa kuwa soko la nje limebanwa na kujikuta wakigiombea wanunuzi wa ndani huku mavuno yameongezeka kutoka  tani millioni 1.2  hadi  tani millioni 1.8. Wamesema wale wanaokuja kununua kutoka nje wamekuwa wakiwekewa vikwazo hivyo ni vyema wakaruhusiwa. Wakizungumza kwenye  mafunzo  ya usindikaji wa zao la mpunga  yaliyoandaliwa  na Baraza la…

Read More

Halmashauri zinazolima mkonge zatakiwa kuanzisha vitalu vya miche

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAZIRI WAZIRI MKUU ATOA AGIZO UENDELEZAJI ZAO LA MKONGE *Halmashauri zinazolima mkonge zatakiwa kuanzisha vitalu vya miche WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa akili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kupunguza tatizo la upungufu wa mbegu. Pia, Waziri…

Read More

Halmashauri zinazolima mkonge zatakiwa kuanzisha vitalu vya miche

KOROGWE: 20.1.2021 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa akili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kupunguza tatizo la upungufu wa mbegu.  Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI Mlingano ili kukiwezesha kupanua…

Read More

Majaliwa ataka halmashauri zianzishe vitalu vya mbegu za mkonge

MUHEZA: 20.01.2021 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote zinazolima zao la mkonge kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche bora ya mkonge na kuigawa kwa wakulima ili kufufua mashamba zaidi na kuongeza uzalishaji zao la mkonge nchini. Ametoa agizo hilo leo wakati alipozindua rasmi zoezi la ugawaji miche bora ya mkonge iliyozalishwa katika kituo cha Utafiti wa zao la mkonge…

Read More

Tani 36,298 za katani zazalishwa 2020

MUHEZA 20.01. 2021 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema mwaka 2020 uzalishaji wa mkonge nchini ulikuwa ni tani 36,298 huku malengo yakiwa ni kuzalisha tani 42,286 kwa mwaka huo. Hata hivyo alisema katika kipindi cha 2020-2025 Bodi ya Mkonge inampango wa kuongeza uzalishaji na kufikia tani 120,000 kwa mwaka. Alisema hayo leo wakati wa kikao cha waziri Mkuu…

Read More

Uzalishaji kapunga wapanda ,aksante kwa teknolojia mpya

MBARALI 8.7.2018 MATUMIZI ya teknolojia za kisasa kumewezesha uzalishaji katika mradi wa Kapunga kuongezeka na kufikia wastani wa asilimia 6.5 ya uzalishaji kwa hekta moja. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa rasilimali watu wa Kampuni ya Kapunga, Fatma Ally wakati akielezea maendeleo ya mradi huo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki. Alisema kitakwimu hali ya uzalishaji wa mpunga imeongezeka…

Read More