January 20, 2021
by Kilimokwanza
KOROGWE: 20.1.2021 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa akili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kupunguza tatizo la upungufu wa mbegu. Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI […]
January 20, 2021
by Kilimokwanza
MUHEZA: 20.01.2021 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote zinazolima zao la mkonge kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche bora ya mkonge na kuigawa kwa wakulima ili kufufua mashamba zaidi na kuongeza uzalishaji zao la mkonge nchini. Ametoa agizo hilo leo wakati alipozindua rasmi zoezi la ugawaji miche bora ya mkonge iliyozalishwa katika kituo cha Utafiti […]
January 20, 2021
by Kilimokwanza
MUHEZA 20.01. 2021 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema mwaka 2020 uzalishaji wa mkonge nchini ulikuwa ni tani 36,298 huku malengo yakiwa ni kuzalisha tani 42,286 kwa mwaka huo. Hata hivyo alisema katika kipindi cha 2020-2025 Bodi ya Mkonge inampango wa kuongeza uzalishaji na kufikia tani 120,000 kwa mwaka. Alisema hayo leo wakati wa […]
January 19, 2021
by Kilimokwanza
MBARALI 8.7.2018 MATUMIZI ya teknolojia za kisasa kumewezesha uzalishaji katika mradi wa Kapunga kuongezeka na kufikia wastani wa asilimia 6.5 ya uzalishaji kwa hekta moja. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa rasilimali watu wa Kampuni ya Kapunga, Fatma Ally wakati akielezea maendeleo ya mradi huo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki. Alisema kitakwimu hali ya […]
January 18, 2021
by Kilimokwanza
NACHINGWEA 18.1.2021 BAADA ya minada 23 mkoa wa Lindi umefunga rasmi msimu wa korosho 2020 na kuanza kujiandaa na msimu wa ufuta. Msimu huo umemalizika baada ya kufanyika kwa mnada wa mwisho kwa wakulima wa Liwale kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha Ruangwa, Nachingwea na Liwale (Runali). Mnada huo wa 13 kwa Runali ni mnada […]
January 15, 2021
by Kilimokwanza
IFAKARA 15.01.2021 Wizara ya Kilimo kupitia mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (ERPP) imefanikiwa kukamilisha miradi kumi na moja iliyopo mkoani Morogoro na itakabidhiwa kwa wakulima mwisho wa mwezi huu. Hayo yamebainishwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati alipozungumza na wakulima wa kijiji cha Msolwa Ujamaa Halmashauri […]
January 5, 2021
by Kilimokwanza
Na Beda Msimbe “Kiukweli kilimo cha maharage ni kipya katika maeneo hayo. Hapo zamani mazao ambayo wakulima walizoea kulima ni karanga,njugu na mbaazi” Maharage ni zao maarufu zaidi duniani kati ya mazao mengine ya jamii ya mikunde. Maharage yalifika Tanzania miaka mia tatu (300) iliyopita. Nchini Tanzania na sehemu kubwa ya Afrika Mashariki, maharage yanazalishwa […]
December 24, 2020
by Kilimokwanza
LIWALE:24:12:2020 JUMLA ya kilo 1,717,665 za korosho za daraja la kwanza na la pili ziliuzwa katika mnada 11 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ruangwa, Nachingwea na Liwale (RUNALI) uliofanyika mjini Liwale hivi karibuni.Mauzo hayo yalifanywa kwa mfumo wa sanduku na mauzo ya mtandao (TMX) ambapo kampuni Baada ya kampuni 14 zilijitokeza kununua. Mnada huo […]
December 20, 2020
by Kilimokwanza
Dodoma Waziri wa Kilimo Prof Adolf Mkenda amesema kipaumbele chake ni kuona wakulima wanaongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao nchini kwa kutumia eneo dogo kuzalisha mazao mengi zaidi na kukuza uchumi wa kaya na taifa. Waziri wa Kilimo amesema hayo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga katika hafla iliyofanyika makao […]
December 11, 2020
by Kilimokwanza
Na Mwandishi Wetu, Mvomero 11.12.2020 Shirika la Bima la Taifa limewalipa wakulima watano wa Mvomero jumla ya shilingi milioni 23 ikiwa ni fidia ya mazao yao kuharibiwa na majanga ikiwemo mafuriko yaliyoharibu mashamba yao ya mpunga na mahindi msimu uliopita wa kilimo. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ndiye aliyekabidhi hundi ya shilingi milioni […]