“Wakati umefika kwa watanzania kujifunza na kuzalisha kwa kasi korosho ghafi si kwa kwenda kuziuza zilivyo bali kuzichakata ili kupata mahitaji mbalimbali ambayo yatasaidia bei ya korosho na mazao mengine mtambuka kuwa juu na kufaidisha jamii na taifa kwa ujumla”
Na Beda Msimbe
MLIPUKO wa ugonjwa wa Covid 19 umeleta kizaazaa katika masoko mengi duniani ikiwamo soko la korosho . Pamoja na kusababisha bei ya korosho ghafi na korosho karanga kuwa za chini, matokeo yake yanatoa haja ya kuwapo na umuhimu wa pekee wa kufuatilia uchakataji wa zao hilo ili kutanua wigo wake kisoko.
Kwa kuwa bei ya korosho ghafi katika soko la dunia inategemea sana mwenendo wa bei ya korosho karanga ni dhahiri Covid 19 imesababisha kupungua kwa mauzo yake kutokana na kupungua kwa ulaji katika masoko makuu ya India, Vietnam pamoja na masoko ya China, Ulaya, Marekani na Mashariki ya Kati.
Aidha bei ya korosho karanga nchini India na Vietnam kwa madaraja mbalimbali ilishuka kwa kiasi kidogo kuanzia Machi hadi Julai 2020 ukilinganisha na mwezi Machi hadi Julai mwaka 2019 na kuleta kizaazaa katika soko la korosho ghafi.
Katika mazungumzo na Dk Fotunatus Kapinga wa kituo cha utafiti wa Kilimo cha Naliendele, Mtwara, alisema kutokana na Covid 19 wamebaini kwamba wakati umefika kwa watanzania kujifunza na kuzalisha kwa kasi korosho ghafi si kwa kwenda kuziuza zilivyo bali kuzichakata ili kupata mahitaji mbalimbali ambayo yatasaidia bei ya korosho na mazao mengine mtambuka kuwa juu na kufaidisha jamii na taifa kwa ujumla.
Dk Kapinga anasema matumizi ya mazao ya korosho hapa nchini ni madogo sana kulinganisha na mahitaji halisi.
Anasema hapa nchini korosho ghafi inapewa kipaumbele kuliko mabibo ambayo yanaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwamo juisi.

“Kwenye ghorosho ghafi tunachothamini ni korosho karanga ambaoz kwa uzito ni wastani wa asilimia 20-25 tu ya korosho ghafi” anasema Dk Kapinga na kuongeza kwamba ngozi laini (testa) ambayo ni asilimia 2 na maganda ambayo ni asilimia 75-80 ya uzito wa korosho ghafi hazihesabiwi kwenye thamani ya korosho.
Anasema kiujumla kuna matumizi madogo ya mazao ya korosho hapa nchini na kufanya kutegemea zaidi mauzo ya korosho ghafi ambayo kwa sasa soko lake limeyumba.

Anasema kwenye korosho pia kuna mafuta ya maganda (CNSL) ambayo hatutumii na kama kuna matumizi ni madogo huku makapi ya maganda hayatumiki huku ikiwa inajulikana ni chakula kizuri kwa mifugo.
Dk Kapinga anasema kwamba uhamasishaji wa matumizi ya korosho nchini mdogo, ambapo kazi wanazofanya sasa wao kama Naliendele kuonesha kwamba inawezekana kuwa na soko kubwa la korosho na hivyo kuwapo na haja ya upanuzi wa Kilimo chenyewe kutokana na ukubwa wa mnyororo wa thamami.
Historia ya zao hili inaanzia karne ya 16 wakati wareno walipoleta zao hili Afrika Mashariki si kwa sababu ya kupata matunda yake bali kwa sababu ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi.
Kutokana na hali hiyo halikuangaliwa kama zao la biashara.
Akielezea kiundani zaidi kuhusu korosho Tanzania, Mratibu wa zao la korosho katika kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari Naliendele), Dk Geradina Mzena alisema kwamba korosho zilianza kupandwa kwa wingi nchini Tanznaia Badaa ya vita kuu ya pili ya dunia na kuendelea kuongezeka katika miaka ya sitini na uzalishaji kuongezeka kutoka tani 8,000 mwaka 1945 hadi tani 145,000 mwaka 1973/74.
“kiwango hiki kilifanya Tanzania kuwa nchi ya ;ili duniani kuzalisha korosho kwa winvgi ikitanguliwa na Msumbiji” nalisema Dk Mzena.
Hata hivyoi zao hilo lilikuja poromoka hadi tani 16,400 mwaka 1986/87 kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa ubwiriunga.
Hata hivyo Dk Mzena alisema kwamba ugunduzi wa mbegu zenye ukinzani dhidi ya ugoinjwa wa ubwiriunga na ugunduzi wa viuatilifu kutokana na juhudi za taasisi hiyo kulifanya uzalishaji kuongezeka kufikia tani 313,000 katika msimu wa 2017/18.
Pamoja na utafiti wa mazao mengine ya mafuta , Tari Naliendele ina jukumu la kitaifa la kufanya utafiti wa zao la korosho nchini na matokeo ya utafiti wao ndio umekuza zao hilo na sasa wanalipa uwezo wa kuchakatwa.
“Katika kuongeza thamani ya zao la korosho, licha ya kubangua tumefanya utafiti na kupata njia za kuongeza thamani ya korosho kwa kutengeneza bidhaa za korosho kama vile siagi, maziwa,mvinyo na jamu, “ anasema Dk kapinga.
Pamoja na kuifanikiwa katika tafiti kunzia utanuaji wa mikoa inayolima korosho, Tari naliendele imekuwa na kiwanda kidogo cha kufundishia wakulima namna ya kuchakata zao la korosho.
Msimamizi wa kiwanda cha ubanguaji na uongezaji wa thamani wa zao la korosho katika taasisi ya Tari Naliendele- Baraka Zebedayo anasema mkorosho una kila kitu kinachofaa kwa chakula na kinywaji kwa mwanadamu.
Anasema kwenye tafiti zao wamesema kutengeneza fomula zinazofaa kwa ajili ya mvinyo, na juisi na jamu.
“ Likiwa freshi linakuwa hai kwa muda mfupi lakini sisi tumefanikiwa kukausha na kukaa nalo kwa muda mrefu. Huku wanaita chokocho. Hili linaweza kutengeneza mvinyo na pia kitakasa mkono” anasema Baraka.
Anasema si mvinyo pekee lakini pia korosho iliytobanguliwa inaweza kutoa unga wa korosho ambao ukichanganywa na fleva nyingine inaweza kuwa chakula kizuri kwa watoto. Aidha unga huo unaweza kuchanganywa na ngano na kutoa chapati nzuri, andazi na kadhalika.
Pia maziwa ya korosho yanayotolewa katika karanga yana ladha na pia vitamini na protini kama yalivyo maziwa ya ng’ombe.
“Hapa sasa hivi kwa kweli tunatathmini muda wa kukaa katika usafirishaji na pia katika uhai wake. Haya maziwa unaweza kuyatengeneza kuwa mtindi kwa kuwa na virutubisho vinavyotakiwa kutengeneza mtindi,” anasema Baraka.
Lakini pia anasema maziwa haya yanaweza kuwekwa fleva mbalimbali na hivyio kuchangia ukuaji wa uchumi mtambuko.
Anasema kituo hicho kwa sasa kipo tayari kwa amafunzo na ndio maana wana kiwanda kidogo na wangelipenda wanaotaka kujikita katika kutengeneza bidhaa mbalimbali kwenda kujifunza na kuelekezwa aina ya mashine zinazofaa kwa kazi hizo.
“Tunafanya hivi kwa kuwa korosho ina matumizi mengi na kama wananchi wakichukua bidha ahizi na kuzitumia maana yake hakuna sababu za kuhangaika na soko la nje, soko la ndani na Afrika mashariki ni kubwa” anasema Baraka.
Kuwepo kwa bidhaa tofauti zinazoweza kusaidia kuinua bei ya korosho kumepokelewa vyema na wakulima mbalimbali.
Mkulima wa Korosho wa Liwale, Hassan Mpako, anasema wananchi wakijikita katika kupata bidhaa mbalimbali zinazotokana na korosho ni dhahiri matumizi hayo ya ndani yataweka sawa bei ya korosho na kilimo chake kitakuwa na faida kubwa.
“Hiki Kilimo tukifundishwa namna ya kutengeneza hizi bidhaa, tukachakata korosho kuanzia bibo hadi korosho karanga, tutaku wa hatuna sababu ya kuwa na kilio cha fedha, fedha ipo humu” anasema Mpako.
Kwa sasa mikoa inayolima korosho ni 20 na hivyo kufanya katika miaka mitatu ijayo Tanzania kuwa na malighafi ya kutosha kwa bidhaa mbalimbali ikiwa pamoja na kemikali inayotumika kutengeneza kutakasa mikono ambayo kwa sasa inaagizwa kutoka nje.
“Kuna ethanol nyingi kutoka katika mabibo na tutakapoweza kuwa na viwanda vidogo na vya kati tunaweza kutengeneza vitakasa mikono vya kwetu wenyewe” anasema Baraka.
Kwa dk kapinga, korosho ni mpango mzima hasa katika kutengeneza ajira kuanzia kwa mkulima, muuzaji, mtengeneza vifungashio, wahckataji na hata wanaolima mazao yanaweza kutumika kama fleva.
Anasema korosho ina virutubisho vingi ikiwamo madini ya chuma, magneziamu, zinki na kadhalika na hata vitamisi C ambayo ni mara 5 ya ile iliyomo katika chungwa.
2 comments
Habari naitwa Vedastus Karume ningependa kujua namna ya kutengeneza Mvinyo wa korosho
Habari Vedastus, karibu sana. Mvinyo wa korosho ni biashara nzuri kabisa, hasa hapa Tanzania ambapo mabibo (matunda ya mkorosho) mengi hupotea bure huku korosho zenyewe zikivunwa. Hebu nikuelekeze hatua kwa hatua.
Kwanza, ufafanuzi muhimu: mvinyo hautengenezwi kutoka kwenye korosho (kokwa) bali kutoka kwenye **bibo** — lile tunda laini jekundu au la njano lililoshikamana na korosho. Hilo ndilo lina maji matamu yanayofaa kuchachuka.
## Vifaa na malighafi
Utahitaji mabibo mabivu, sukari, hamira ya mvinyo (wine yeast — aina ya EC-1118 ni nzuri, lakini hamira ya kawaida ya mkate inaweza kufanya kazi kwa kuanzia), ndoo au pipa la plastiki lenye mfuniko (fermentation bucket), chupa au gallon ya kuchachushia, na kifaa kidogo kinachoitwa *airlock* kinachoruhusu hewa chafu kutoka bila kuingiza hewa ya nje. Kama unaweza kupata kipima-sukari (hydrometer) na vidonge vya Campden (sodium metabisulphite), vitakusaidia sana kuboresha ubora.
## Hatua za kutengeneza
**1. Kusafisha na kuandaa mabibo.** Chagua mabibo mabivu yasiyo na uozo, ondoa korosho, kisha osha vizuri kwa maji safi.
**2. Kupunguza uchachu/ukakavu (astringency).** Hii ndiyo changamoto kubwa ya bibo — lina tannin nyingi zinazoacha ukakavu mdomoni. Chemsha au anika mabibo kwa mvuke (steam) kwa dakika 5–10, au kamua maji kisha yaache yatulie usiku mzima na uchuje sehemu ya juu safi. Hii hupunguza uchungu.
**3. Kukamua maji.** Ponda mabibo na ukamue maji. Chuja kwa kitambaa safi ili kuondoa makapi.
**4. Kuongeza sukari.** Maji ya bibo yana sukari ya asili kiasi cha 10–12% pekee, hayatoshi kupata mvinyo wenye nguvu. Ongeza sukari hadi ufikie kiwango cha takriban gramu 220–250 kwa lita moja ya maji. Ukitumia hydrometer, lenga usomaji wa karibu 1.090 (utapata mvinyo wa takriban asilimia 12 ya kileo).
**5. Kuua vijidudu.** Kama una vidonge vya Campden, weka kidonge kimoja kwa kila lita 4–5 za juisi, koroga, na uache kwa masaa 24 kabla ya kuweka hamira. Hii huua bakteria wabaya.
**6. Kuweka hamira.** Changanya hamira na maji vuguvugu kidogo (siyo ya moto) iamke kwa dakika 15, kisha imimine kwenye juisi na ukoroge vizuri.
**7. Uchachushaji wa kwanza (primary fermentation).** Funika ndoo, weka airlock, na uweke mahali penye joto la kawaida (nyuzi 20–28). Utaona mapovu yakitoka — hii ni dalili nzuri. Uchachushaji huu huchukua siku 5–7.
**8. Kuhamisha (racking).** Baada ya mapovu kupungua, hamishia mvinyo kwenye chombo kingine safi (gallon yenye airlock), ukiacha mashapo chini. Hii ni uchachushaji wa pili, huchukua wiki 2–4.
**9. Kusafisha na kuzeesha (aging).** Rudia kuhamisha kila yanapotokea mashapo. Mvinyo ukikaa miezi 2–6 ladha yake huongezeka sana.
**10. Kuweka kwenye chupa.** Mvinyo ukiwa safi na haufanyi mapovu tena, weka kwenye chupa zilizosafishwa na uzifunge vizuri.
## Vidokezo vya muhimu
Usafi ndio kila kitu — vifaa vichafu huleta siki badala ya mvinyo. Hakikisha kila kifaa kimesafishwa vizuri. Pia, epuka chuma na alumini; tumia plastiki ya chakula, glasi au chuma cha pua (stainless steel) kwa sababu asidi ya bibo huharibu vyuma vya kawaida.