Runali wauza kilo milioni 1.7 za korosho mnada wa 11
LIWALE:24:12:2020 JUMLA ya kilo 1,717,665 za korosho za daraja la kwanza na la pili ziliuzwa katika mnada 11 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ruangwa, Nachingwea na Liwale (RUNALI) uliofanyika mjini Liwale hivi karibuni.
Mauzo hayo yalifanywa kwa mfumo wa sanduku na mauzo ya mtandao (TMX) ambapo kampuni Baada ya kampuni 14 zilijitokeza kununua.
Mnada huo ambao unakuwa ni wa 21 kimkoa na wa 11 kwa Chama Cha Ushirika cha Runali korosho za daraja la pili zilikuwa kilo 465,004. Katika mnada huo bei ya juu kwa kilo ilikuwa Sh 2,350 na ya chini ilikuwa Sh 2,250.
Aidha iilikubaliwa kwamba bei ya juu ya korosho daraja la pili ilikuwa ni sh 1,595.
Kampuni zilizoshiriki kwa sanduku na TMX na kushinda ni Udhaya, MGM, Budang na Megnacio(TMX).
Kwa upande wao baadhi ya Wakulima walishiriki katika mnada huo wa 11 uliofanyika katika kituo cha malipo cha Runali wilayani Liwale walieleza kuridhishwa na bei hizo kutokana na kipindi kilichopo huku wakiendelea kusisitiza malipo yao yafanywe kwa haraka ili kuwahi maandalizi ya mashamba yao.
Wakulima hao Amina Kanduru, Mohamed Mtwiku wote wa Liwale walipongeza namna minada ilivyoendeshwa na kuomba zaidi kwmaba fedha zao zilipwe kwa wakati.
Walishukuru utaratibu wa Runbali wa malipo kupitia vituo vyao hali ambayo imefanya chama chao kuwajibika zaidi kwa wanachama wake.
Naye,Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Lindi Edmund Massawe akizungumza alieleza kuridhishwa na taratibu za minada zinavyoendela ikiwemo malipo ya haraka kwa Wakulima .
,Meneja wa Runali Jahida Hassan alielezea kuridhishwa na watendaji wa Runali wanavyofanya kwa kasim kushughulikia malipo ya wakulima lakini na yeye alitoa msisitizo kwa Wakulima kulipa madeni ya pembejeo ili kuweza kukopeshwa tena kwa msimu ujao.
Wakati huo Mwenyekiti wa RUnali , Hassan Mpako amewataka Wakulima wa zao la korosho kutumia mvua zilizoanza kunyesha katika mkoa wa lindi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ikiwemo Ufuta,Choroko na mbaazi ili kuondokana na tatizo la chakula pamoja na kufanya mzunguko wa pesa walizolipwa kuwa na tija kwa siku zijazo.
Mpako alisema hayo akifunga kikao cha mnada wa 11 wa mauzo ya zao la korosho kwa Wakulima wa chama kikuu cha wilaya za Ruangwa ,Nachingwea na Liwale .
Mpako alieleza kuwa Kutokana na malipo kufanywa kwa wakati ipo haja kwa Wakulima kujiwekea akiba ikiwemo maandalizi ya kilimo kwa msimu ujao,.
mwisho
—