Search Agricultural Insights

Menu

🌟 Mjadala: ‘Mbinu za Kukabiliana na Visumbufu na Magonjwa ya Embe’

📅 Tarehe: 12 Januari | ⏰ Saa kumi jioni

🍋 Agribusiness East Africa, kwa ushirikiano na Chama cha Wakulima wa Maembe Tanzania (AMAGRO), COPRA, TOSCI, SAGCOT, TAHA, Diligent Consulting Limited, na Nature Ripe, wanakuletea mjadala muhimu unaozingatia mbinu za kukabiliana na changamoto zinazokumba zao la embe, ikiwemo visumbufu na magonjwa mbalimbali yanayoathiri mazao haya.

Katika mjadala huu, tutajikita zaidi kwenye:

  • Utafiti wa Kisayansi na Ushirikiano: T utaangalia jinsi utafiti wa kisayansi unavyoweza kusaidia kutambua na kukabiliana na visumbufu na magonjwa ya embe, na umuhimu wa ushirikiano baina ya watafiti, wakulima, na wadau wengine.
  • Mbinu za Kisasa: Tutachambua teknolojia mpya na mbinu za kisasa zinazotumika katika kudhibiti visumbufu na magonjwa haya, kama vile matumizi ya biopesticides na mbinu za kilimo hai.
  • Mafunzo na Uwezeshaji wa Wakulima : Tutajadili umuhimu wa kutoa mafunzo na maarifa kwa wakulima kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto hizi, kuimarisha mifumo ya kinga ya mazao, na kuongeza uzalishaji wenye tija.
    🔗 Jiunge nasi katika tukio hili la kipekee na uwe sehemu ya majadiliano yatakayokuza uelewa na kushirikisha uzoefu baina ya wadau mbalimbali wa kilimo cha maembe.

👉 Usikose! https://www.clubhouse.com/invite/y32S7lg0ZpbVVzvnE7aDl2NbQr4lSnjvA43:Z3RrleYOK79kPel0OTAmMAzVP4bUGYe8i8-0VuR7-7I

Kilimokwanza Assistant ×
Hello! I can help you find information. What would you like to know?
Kilimokwanza Assistant ✕
Hello! How can I help you learn about Kilimokwanza today?