Mama Seki: nimeigia mikataba na wakulima wadogowadogo kuniuzia mahindi, Ruvuma na Iringa

Na Mwandishi wetu

BARAKA kubwa katika kazi za mikono hutegemea zaidi namna unavyofanya menejimenti ya program unayoifanya na mkazo unaotilia ili uweze kutoboza. Hata kama utaletewa mafunzo ya namna gani kama usipotia nia na kuweka mpango wako katika utekelezaji huwezi kufanikiwa.

Hayo ni sehemu tu ya baadhi ya maneno ambayo yamezungumwa katika mahojiano na msagishaji wa mahindi na kuzalisha bidhaa ya unga, Rita Seki, anayefanyia kazi yake mkoa wsa Iringa.

Rita Seki ni zao na kazi kubwa inayofanywa na Taasisi ya mapinduzi ya Kijani barani Afrika (AGRA) ya kuchochea uwapo wa masoko kw abidhaa za wakulima.

AGRA ikiwa katika awamu ya nne ya kuchochea masoko imetengeneza aina ya jkukwaa linaloratibu mambo yanayofanyika katika sekta ya kilimo ili kuichagiza zaidi.

Rita Seki anayezalisha bidhaa ya unga wa mahindi ijulikanayo kama Super Seki ikiwa na virutubisho  anasema alianza kazi ya kusaga mahindi na kuuza kwa debe mbili tu lakini sasa anauwezo wa kununua zaidi ya tani 200 za mahindi kutoka eneo moja kwa mkupuo na akazisaga akichanganya na virutubisho na kuiuza katika ujazo mbalimbali.

Mwenyewe anasema kwamba kwa sasa ameingia mkataba na wakulima katika vikundi na hasa wanawake kununua mahindi yao na kuyaleta katika kiwanda chake kilichopo Iringa mjini.

Akizungumza wakati ametembelewa na rais wa Taasisi ya mapinduzi ya kijani barani Afrika, AGRA, Dk Agnes Kalibata alisema kwamba  taasisi hiyo inamuunga mkono kwa kumpatia fedha za kujenga ghala.

Anasema wakati wao (AGRA) wanatoa kiasi cha shilingi milioni 40 kumwezesha kujenga ghala la kuhifadhia mahindi kiasi cha tani 10,000, Taasisi ya USAID kupitia mradi wake wa Nafaka wamempatia mashine ya kuongeza virutubisho katika sembe anayoizalisha.

Kwa kuwa na uwezo wa kuzalisha sembe na hivyo kuhitaji malighafi yake, mahindi, maana yake anaongeza wigo wa mkulima kuuza mazao yake.

Mama Seki anasema ameigia mkataba na wakulima kumpatia mahindi, hivyo wakulima katika maeneo kadha ya Ruvuma na iringa wana uhakika na soko kwani mwanamama huyo anachukua mahindi yao kwa ajili ya sembe.

“mimi sikusoma lakini, katika biashara najua nini ninachofanya” anasema mama Rita katika mazungumzo yake,m kwenye mkutano mkubwa wa wazi wa wadau katika jukwaa huru la Ihemi-Ludewa  mkoani iringa ambalo linawezeshwa kielimu na AGRA.

Akiwa katika mkutano huo ofisi za Mkuu wa mkoa wa Iringa, mama Seki anasema anajivunia kukua kwa biashara yake na sasa anataka kufungua njia kwa soko la kitaifa na kimataifa hasa ukanda wa Afrika Mashariki.

Sembe yenye virutubisho anayoisindika katika kiwanda chake kwa sasa anauza mikoa ya Lindi, Mtwara ,Iringa, Mbeya, Dar es salaam, Dodoma, Ruvuma  na Iringa.Pia sembe hiyo inasambazwa katika shule mbalimbali.

Dk Kalibata alimpongeza mdada huyo na kusema katika sekta ya kilimo wanahitajika wanawake wa aina hiyo wengi ili kuweza kutanua zaidi soko na kujenga utajiri unaotakiwa kwa wakulima.

Mkuu wa AGRA kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Profesa Nuhu Khatibu alisema mafanikio ya mwanamama huyo ni kielelezo tosha cha juhudi za AGRA za kuunganisha makundi mbalimbali kutatua changamoto za kilimo.

Jukwaa likitumika kama sehemu ya kukutanisha wadau chini ya uongozi wa serikali ambao ndio wenye utaalamu na sera mafanikio makubwa yatapatikana, kwani lengo la kuwa na jukwa ni kuwaweka karibu wadau wote .

Mama Seki kwa kuwa na kiwanda maana yake anasaidia wakulima kuwa na eneo la kuuzia nafaka zao, lakini kikubwa zaidi kuwa na uhakika wa soko ili waweze kuzalisha kwa wingi zaidi na hivyo kuongeza tija na faida.

“Lengo la kuwa na jukwaa ni kutambua mahitaji na kujua namna ya kukidhi mahitaji hayo kw amanufaa ya wakulima nawawekezaji katika sekta ya kilimo” anasema Profesa Nuhu akielezea maoni ya mama Seki kwamba Jukwaa hilo limemsaidia sana.

Mama Seki anasema jukwaa limemuunganisha na wakulima ambao nao kwa upande mwingine wanampatia mahindi bora ya kusindika kwa chakula.

Akiwa anachukua mahindi katika makundi 32 huku eneo la Mwaking’ombe akitwaa tani 200 ambaoz tayari wamekubaliana na wakulima, mama Seki  was per Seki samba anasema anatyarajia kuongeza uwezo kufikia tani 5000 za nafaka baada ya kuunganishwa na watu wa Benki.

Taasisi ya Nafaka ya Shirika la USAID ndilo lililompatia elimu, mashine ya virutubisho na kumpigia chapuo Benki.

Kutokana na kukua kwa mtaji taasisi moja ya kifedha mkoani iringa imepanga kuhakikisha kwamba inampa uwezo zaidi wa kutanua ghala lake na pia kumpa fedha za kuwalipa wakulima katika manunuzi ya mahindi.

Katika mazungumzo yake na wadau mbalimbali mama Seki alisema kwamba ameingia mkataba wa kimaandishi na wakulima kadhaa wakiwemo walio ndani ya vikundi kwa ajili ya kuwa na uhakika wa mahali pa kupata mali ghafi yake.

Mmoja wa wakulima ambaye yumo katika orodha yake ni Victory Mhanga wa kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa halmashari ya Iringa.

Mkulima huyo ambaye pia anauza mazao yake kwa pamoja katika ghala la chama cha msingi cha magulilwa amcos anasema kwamba mama seki ameingia mkataba na amcos yao na wamekuwa na uhakika wa soko.

Anasema kwa kufanikisha soko , wakulima kama yeye wanakuwa na nafasi kubwa ya kupanua kilimo ili kukiwezesha kuleta tija inayokusudiwa na faida tarajiwa.

“kilimo cha kisasa ni ghali lakini kinalipa” anasema mkulima huyo ambaye alisema pamoja na kuanza kuona mafanikio katika kilimo cha mahindi , fedha zake zitamsaidia kupata mtaji wa kulima soya ambayo nayo ataitumia kwa ajili ya kutengeneza chakula cha mifugo na chake.

Wakati mama Seki anawawezesha wakulima kuwa na soko, yeye pia anakuwa mmoja wa watu muhimu sana katika kuleta mnyororo wa thamani kwa kuwa karibu na wakulima. Kupanda kwa uwezo wa kulima kutamsaidia na yeye kuwa na uhakika wa mali ghafi ili anapioingia soko la kimataifa ajue anapeleka nini.

 Utengenezaji wa sembe una kazi nyingi ikiwamo cha  kumenya punje. Mabaki yanayotokana na umenyaji huo (pumba) hutumika kama chakula cha mifugo kwa watu wanaonunua.

Mshauri wa kilimo mkoa wa iringa, Grace Macha alisema kwamba kumekuwepo na maendeleo makubwa katika mradi wa Ihemi Ludewa wa uratibu, ambapo kwa sasa kuna ongezeko la tija kutokana na kuwapo kwa wafabnyabiashara wawekezaji, wafanyabiashara wanauza pembejeo na pia kuwapo kwa soko.

Alisema Mama Seki amekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutumia mifumo mbalimbali anayojifunza katika mikutano ya pamoja ambayo huangalia masuala ya kilimo na matokeo yake.

Alisema mafanikio ya mama Seki ya kuwa na kiwabnda cha kusagisha sembe tena yenye virutubisho yanafanya yeye ahitaji mahindi na kutokana na ongezeko la mahitaji, wakulima walioingia mkataba naye nao wanafaidika.

mwisho–