Kituo cha huduma kwa wateja kwa wakulima chazinduliwa

WAZIRI wa kilimo Hussein Bashe amezindua kituo cha huduma kwa wateja ambapo wakulima watapata nafasi ya kupiga simu  bure Ili kupata taarifa na kuuliza maswali yanayohusiana na kilimo lengo likiwa ni kuwafikia wakulima popote walipo Nchini.


Sifa Lubasi

“Mkulima yoyote popote alipo Tanzania atapiga simu atauliza maswali ,atasikilizwa na kupata majibu,” alisema.

Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho uliofanyika Jijini hapa.

Alisema jambo hilo ni mwanzo wa kuelekea hatua kubwa ya mafanikio ambapo wakulima watakuwa wakipata  taarifa ya mazao gani yanatakiwa sokoni Ili waweze kulima.

Bashe  alisema wakulima watapiga  bure namba ya huduma kwa wateja ambayo ni 0733800200 na kutaka Watendaji kuitangaza namba hiyo Ili kila mkulima aifahamu.

Alisema kuwa awali walikuwa wakisikiliza matatizo ya wakulima kwa njia ya ujumbe mfupi kwa njia ya simu (sms) lakini sasa yatasikilizwa kwenye simu .

“Tutakuwa na mfumo unaotunza taarifa za wateja ambazo kama swali halijajibiwa muda huo litapata fursa ya kuijbiwa, baada ya dakika kadhaa” alisema.

Alisema kuwa baada ya mfumo wa huduma kwa wateja kukamilika kama Nchi lazima kuwe na kitengo kilichosajiliwa cha masoko  kuangalia bei kwenye soko zinakwendaje .

” Ifike mahali tuwe na kitengo chenye nguvu cha kuingilia soko Ili kufanya mazao yetu ya we na ushindani kwenye soko ,lazima hii kazi ifanywe na watu wa masoko kuwa soko la ufuta litakuwa hivi, la mbaazi hivi Ili hata wakilima wasipate shida ya masoko,” alisema.a

Waziri Bashe aliahiza Kituo hicho kufanya Kazi masaa 24 na kuwe na mfumo unaotunza taatifa.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde alisema kuwa Kazi kubwa imefanyika katika kuiweka Wizara ya Kilimo kiganjani.

Alisema kuwa mkakati uliopo ni kuanzishwa kwa channel maalum kwa ajili ya Kilimo.

Alisema kuwa kupitia Kituo cha huduma kwa wateja wakulima watapata taatifa za kilimo kila siku na wakulima wengi watafikiwa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Andrew Masawe alisema kuwa kupitia mfumo wa M, Mobile Kilimo (M-Kilimo) nikiwa ni teknolojia ya kutumia simu ambayo imelenga kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kuyafikia masoko ya mazao yao kwa njia ya simu zao za mkononi. Hii itawafanya waweze kuyafikia masoko hasa hasa wanunuzi wa bidhaa na mazao yao ya kilimo pasipo kupitia adha ya kuyasafirisha mazao hayo kwenda masokoni.

Alisema kuwa kupitia mfuko.huo mpaka sasa jumla ya wakulima milioni 5,5 wamesajiliwa kwenye Hifadhi data (data base) huku wakisajili wauzaji wa Mazao nje ya Nchi  3905.

Masawe alisema  mpaka sasa tayari wametatua changamoto 60,120 za wakulima ambazo wamezirusha katika kitengo cha huduma kwa wateja.

“Nikuhakikishie huduma hii utaleta matunda mazuri kwa wakulima,”alisema  alisema katika kufanikisha Ajenda ya kuhakikisha kilimo.kinakua kwa asilimi.10 ifikapo mwaka 2030 watakuwa karibu na wakulima . Mwisho